Latest News

  • Home
  • stories
  • cdn-cgi

MRADI WA BIOANUWAI WAENDELEA KUTEKELEZWA MWAMBESI

Mwambesi, Ruvuma – Juni 2025

Wawakilishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais, wamefanya ziara ya ukaguzi katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Mwambesi, Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma, ili kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuwai ya Misitu ya Mazingira Asilia dhidi ya Matishio ya Mabadiliko ya Tabianchi.

Katika ziara hiyo, wajumbe wametembelea eneo la ujenzi wa jengo la utalii, jengo la ulinzi, pamoja na geti la kuingilia hifadhi, ambapo mradi huo tayari umeanza kutekelezwa na umefikia asilimia 10 ya kazi yote. Mradi unatekelezwa chini ya usimamizi wa Brakel Company Ltd kwa gharama ya Shilingi milioni 211, na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 25 Oktoba 2025.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mkuu wa Manunuzi kutoka TFS Makao Makuu, Bw. Fridolin Matembo, alisema:

“Tunaipongeza kampuni kwa kuanza vizuri kazi hii. Kasi ya awali ya ujenzi imeridhisha, lakini tunasisitiza iongezwe ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.”

Mradi huu wa Bioanuwai ni sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TFS na Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kushirikiana na UNDP na ufadhili wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF). Unalenga kuimarisha miundombinu ya uhifadhi, kuboresha huduma za misitu kwa jamii, na kuchochea utalii wa kiikolojia katika maeneo ya hifadhi ya asili.

MRADI WA BIOANUWAI WAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA UHIFADHI – PINDIRO

Kilwa, Lindi – Juni 2025

Kamati ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuwai ya Misitu ya Mazingira Asilia dhidi ya Matishio ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imefanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Pindiro, Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi, kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya uhifadhi pamoja na kukabidhi vifaa vya kazi.

Mradi wa ujenzi unaoendelea ndani ya hifadhi hiyo umefikia asilimia 46, ukihusisha jengo la utalii, vyoo, jengo la mlinzi, na geti la kuingilia, kwa gharama ya Shilingi milioni 297, chini ya mkandarasi Strider Engineering Ltd. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Oktoba 2025.

Mhandisi Hendry Sanga, ambaye ni mkandarasi wa mradi, alisema kazi inaendelea vizuri na wanaendelea kuzingatia muda wa makubaliano pamoja na ubora wa kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Manunuzi kutoka TFS, Bw. Fridolin Matembo, alisema:

“Tunaipongeza kazi nzuri inayofanywa na mkandarasi. Kasi ya utekelezaji ni ya kuridhisha, na tunasisitiza kwamba mradi huu ukamilike kwa muda uliopangwa na kwa viwango vya ubora vinavyokubalika.”

Katika hatua nyingine ya ziara hiyo, pikipiki mbili zimekabidhiwa rasmi kwa hifadhi hiyo, ikiwa ni sehemu ya vifaa vya kazi vilivyotolewa na UNDP kusaidia shughuli za uhifadhi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mratibu wa Mradi, Bw. Mteleka Someni Lusugu, alisema:

“Pikipiki hizi mbili ni sehemu ya vifaa muhimu ambavyo UNDP ilikabidhi kwa Mheshimiwa Waziri wakati wa uzinduzi wa mradi kule Pugu Kazimzumbwi. Zinaletwa Pindiro kusaidia uratibu wa kazi za uhifadhi na kuongeza ufanisi kwa maofisa wetu walioko kwenye maeneo ya kazi.”

Mradi wa Bioanuwai unatekelezwa kwa miaka sita katika maeneo mbalimbali ya misitu ya asili nchini, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimali misitu, kuongeza ustahimilivu wa jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuboresha miundombinu na huduma za uhifadhi kwa maendeleo endelevu ya wananchi na taifa.

Mradi wa Burefobi wachochea utalii ikolojia katika hifadhi ya misitu Pugu Kazimzumbwi

Na Mwandishi Wetu, Pwani

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umesema maboresho ya miundombinu yanayotekelezwa kupitia Mradi wa Kujenga Ustahimilivu wa Bioanuwai ya Misitu dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Misitu ya Asilia ya Hifadhi Tanzania (BUREFOBI-NFR), yamechochea ukuaji wa utalii ikolojia katika Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Pugu Kazimzumbwi, mkoani Pwani.

Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kufikia lengo la kuongeza idadi ya watalii hadi milioni nane ifikapo mwaka 2030 kupitia uboreshaji wa vivutio na huduma za utalii nchini.

Akizungumza wakati wa ziara ya Mshauri wa Kanda wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Onesimus Muhwezi, Mratibu wa Mradi wa BUREFOBI-NFR ambaye pia ni Mhifadhi Mkuu wa TFS, Someni Mteleka, alisema uwekezaji huo umeongeza mvuto wa hifadhi hiyo kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Alisema kupitia ufadhili wa pamoja wa Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) na UNDP, TFS imetekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya utalii katika hifadhi hiyo, ikiwemo ujenzi wa barabara ya kilomita 12 katika eneo la Kimani–Maguruwe, mabanda mawili ya kupumzikia watalii pamoja na lango la kuingilia hifadhini.

“Uboreshaji huu umeongeza upatikanaji wa huduma na kurahisisha watalii kufikia maeneo mbalimbali ya vivutio ndani ya hifadhi,” alisema Mteleka.

Alibainisha kuwa kati ya mwaka 2020 na 2025, Hifadhi ya Pugu Kazimzumbwi imerekodi ongezeko la wastani wa watalii kwa asilimia 69, hali aliyosema imechangiwa na uwekezaji katika miundombinu ya utalii ikolojia na ushirikiano kati ya Serikali na washirika wa maendeleo.

Kwa upande wake, Muhwezi aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia ufadhili wa washirika wa kimataifa, akisema miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika uhifadhi wa mifumo ya ikolojia, kukuza uchumi wa jamii zinazozunguka hifadhi pamoja na kuongeza mapato yatokanayo na utalii.

Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Pugu Kazimzumbwi ni miongoni mwa hifadhi tisa zinazotekelezwa mradi wa BUREFOBI-NFR, unaolenga kuimarisha ustahimilivu wa bioanuwai ya misitu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi nchini.

Mradi wa Bioanuwai waendelea kuimarisha miundombinu ya uhifadhi

Kilwa, Lindi – Juni 2025

Kamati ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuwai ya Misitu ya Mazingira Asilia dhidi ya Matishio ya Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), imefanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Pindiro, Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi, kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya uhifadhi pamoja na kukabidhi vifaa vya kazi.

Mradi wa ujenzi unaoendelea ndani ya hifadhi hiyo umefikia asilimia 46, ukihusisha jengo la utalii, vyoo, jengo la mlinzi, na geti la kuingilia, kwa gharama ya Shilingi milioni 297, chini ya mkandarasi Strider Engineering Ltd. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Oktoba 2025.

Mhandisi Hendry Sanga, ambaye ni mkandarasi wa mradi, alisema kazi inaendelea vizuri na wanaendelea kuzingatia muda wa makubaliano pamoja na ubora wa kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Manunuzi kutoka TFS, Bw. Fridolin Matembo, alisema:

“Tunaipongeza kazi nzuri inayofanywa na mkandarasi. Kasi ya utekelezaji ni ya kuridhisha, na tunasisitiza kwamba mradi huu ukamilike kwa muda uliopangwa na kwa viwango vya ubora vinavyokubalika.”

Katika hatua nyingine ya ziara hiyo, pikipiki mbili zimekabidhiwa rasmi kwa hifadhi hiyo, ikiwa ni sehemu ya vifaa vya kazi vilivyotolewa na UNDP kusaidia shughuli za uhifadhi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mratibu wa Mradi, Bw. Mteleka Someni Lusugu, alisema:

“Pikipiki hizi mbili ni sehemu ya vifaa muhimu ambavyo UNDP ilikabidhi kwa Mheshimiwa Waziri wakati wa uzinduzi wa mradi kule Pugu Kazimzumbwi. Zinaletwa Pindiro kusaidia uratibu wa kazi za uhifadhi na kuongeza ufanisi kwa maofisa wetu walioko kwenye maeneo ya kazi.”

Mradi wa Bioanuwai unatekelezwa kwa miaka sita katika maeneo mbalimbali ya misitu ya asili nchini, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi wa rasilimali misitu, kuongeza ustahimilivu wa jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuboresha miundombinu na huduma za uhifadhi kwa maendeleo endelevu ya wananchi na taifa.

TFS, UNDP na Ofisi ya Makamu wa Rais watembelea miradi ya uhifadhi Kusini

TFS, UNDP na Ofisi ya Makamu wa Rais watembelea miradi ya uhifadhi Kusini

Masasi – Tunduru, Juni 2025

Wawakilishi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), na Ofisi ya Makamu wa Rais wamefanya ziara ya pamoja katika Kanda ya Kusini kutathmini utekelezaji wa miradi ya uhifadhi ya misitu ya asili na ujenzi wa miundombinu ya uhifadhi.

Ziara hiyo imehusisha ukaguzi wa miradi ya Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuwai ya Misitu ya Mazingira Asilia dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi unaofadhiliwa na UNDP, pamoja na miradi inayotekelezwa kwa kutumia rasilimali za ndani za TFS. Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Hifadhi za Pindiro, Rondo, na Mwambesi katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Katika Hifadhi hizo, wajumbe wamejionea maendeleo ya kazi za ujenzi wa miundombinu ya uhifadhi, ikiwemo vituo vya kulinda misitu, njia za doria na maboma, ambayo inalenga kuongeza ufanisi wa uhifadhi, kuboresha maisha ya jamii na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katika kikao maalum cha tathmini kilichofanyika Masasi, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi kutoka TFS Makao Makuu, Bw. Fridolin Matembo, alisema: “Tunaishukuru UNDP kwa kuendelea kushirikiana nasi katika kutekeleza mradi huu muhimu. Tunasisitiza usimamizi makini wa rasilimali za mradi ili manufaa yake yadumu kwa vizazi vijavyo.”

Kwa upande wake, Bi. Tulalumba Bangu kutoka UNDP Tanzania, alieleza kuridhishwa kwake na mwenendo wa utekelezaji wa mradi huo: “Tumefurahishwa na jinsi kazi zinaendelea. UNDP itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania, hasa kupitia TFS, kuhakikisha masuala ya uhifadhi yanapewa kipaumbele kama njia ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.”

Aidha, wajumbe hao walitembelea ujenzi wa ofisi ya Mhifadhi wa Wilaya ya Tunduru, mradi unaogharamiwa kwa fedha za ndani za TFS. Mradi huo umetekelezwa na mafundi wa ndani kutoka jamii ya eneo husika na umefikia asilimia 65.

Akizungumzia mradi huo, Mratibu wa Miradi wa TFS, Bw. Mteleka Someni Lusungu, alisema: “TFS imejizatiti kutekeleza miradi kwa kutumia rasilimali zetu za ndani. Tunaamini ujenzi wa ofisi hii utaimarisha mazingira ya kazi kwa watumishi wetu na kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.”

Ziara hiyo imelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na wadau wa maendeleo, kuongeza uwazi na ufuatiliaji wa miradi ya mazingira, sambamba na kutathmini changamoto na mafanikio yaliyopatikana.

Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Bioanuwai ni wa miaka sita na unatekelezwa katika misitu ya asili mbalimbali nchini Tanzania, ukiwa na lengo la kuongeza uwezo wa jamii kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kulinda bioanuwai, na kusimamia misitu kwa njia shirikishi na endelevu.